Timu ya Azam Fc leo itashuka dimbani kuvaana na Tanzania Prizons katika muendelelezo wa Ligi Kuu.
Azam Fc watacheza mchezo huo wakiwa na kumbukumbu mbaya ya kutupwa nje kwenye michuano ya kombe la shirikisho Afrika baada ya kuondoshwa na Bahir Dar Kenema ya Ethiopia.
Mchezo wa huo utakaopigwa kwenye dimba la Azam Complex Chamazi utakuwa ni mchezo wa pili kwa timu zote kwenye ligi kuu msimu huu, ambapo mchezo wa kwanza Azam Fc waliichapa Tabora United mabao 4-0 huku Prizons wakilazimisha sare dhidi ya Singida Fountain Gate.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE