Home KITAIFA KISA YAO, KIBWANA APATA WAKATI MGUMU YANGA, KAMWE AFUNGUKA KILA KITU

KISA YAO, KIBWANA APATA WAKATI MGUMU YANGA, KAMWE AFUNGUKA KILA KITU

0
Ally Kamwe

Ofisa Habari wa Klabu ya Yanga, Ally Kamwe amesema kuwa sasa ameelewa kwa nini beki wa kulia na kushoto wa Yanga SC, Kibwana Shomari amesema kwenye nafasi yake kuna kazi kubwa ya kujihakikishia namba.

Kamwe amesema hayo jana Jumapili, Agosti 20, 2023 baada ya kumalizika kwa mechi ya Kombe la mabingwa Afrika kati ya ASAS FC ya Djibouti na Yanga ambapo Yanga walifanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 2-0 katika Dimba la Chamazi.

Kauli hii ya Kamwe inakuja baada ya Yanga kumsajili beki kutoka ASEC Mimosas, Attoula Yao Kouassi ambaye ameonyesha kiwango bora katika mechi chache alizocheza tangu ajiunga na wananchi miezi miwili iliyopita.

“Kibwana aliposti kwamba kazini kwake kuna kazi, sisi tumemuelewa. Kibwana ni mtu wa kazi, ni mchezaji mwenye weredi mkubwa, kwanza anakubali ubora wa mtu aliyeko kwenye nafasi yake kabla ya kushindana naye.

“Hata msimu uliopita wakati unaanza Kibwana hakuwa na namba, lakini Kibwana alicheza nusu fainali zote mbili za Kombe la Shirikisho Afrika, kweli kazini kwake kuna kazi lakini Kibwana ni mtu wa kazi, kwa hiyo kazi itafanyika.

“Kuna siku itafika Gamondi atapanga kikosi hapa, namba 2 ataandika Yao na namba saba ataandika Yao kwa sababu kote anaweza kucheza vizuri, anakimbizwa winga na beki wake,” amesema Ally Kamwe.

Awali Kibwana Shomari kupitia mitandao yake ya Kijamii aliandika; “Kila nikijitahidi mazoezini lakini wapi safari hii kazini kwangu mambo magumu huyu jeshi anakera sasa, ila lawama zangu Nampa rais Eng Hersi kwa nini amenifanyia hivi mimi.”

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here