Home KITAIFA KUMBE AHMED LLY ALIKURUPUKA KUHUSU JEZI YA MKUDE

KUMBE AHMED LLY ALIKURUPUKA KUHUSU JEZI YA MKUDE

0

Jezi namba 20 katika kikosi cha Simba ilikuwa ikivaliwa na kiungo Mwandamizi Jonas Mkude, lakini mwishoni mwa msimu uliopita Simba waliamua kuachana nae.

Kulitokea maneno mengi wakati wa kuachwa kwa Mkude na Simba kwa kujisafisha, kupitia msemaji wake Ahmed Ally walitangaza hadharani kuwa watamuaga Mkude kwa heshima zote siku ya Simba Day, na kubwa zaidi wameamua kuistaafisha jezi namba 20 ambayo ilikuwa ikivaliwa na Jonas Mkude.

Katika Mechi za Kirafiki zilizopigwa siku za hivi karibuni jezi ya Mkude imeonekana kupewa mchezaji mwingine na Mchambuzi wa Soka Jemedari Saidi kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika;

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa klabu ya Simba Ahmed Ally alikurupuka kusema kitu ambacho hakupaswa wala hakuambiwa kukisema pale alipotoa taarifa ya klabu kwamba imeamua kustaafisha jezi namba 20 iliyokuwa inavaliwa na Jonas Mkude, au Simba SC ilikurupuka kupanga jambo ambalo haikulitafiti vyema na kujua athari zake chanya na hasi kwa jamii na kwao binafsi.

Inawezekana pia kwamba mipango imebadilika baada ya kuwasikia Yanga ambao ni wajiri wapya wa Jonas Mkude kwamba hawatomruhusu kuagwa na Simba siku ya Simba day, au wao wenyewe wameingia kinyongo baada ya Mkude kusajili Yanga na kuonekana akiibusu jezi ya Yanga kitu ambacho kinaweza kutafsiriwa kama usaliti mbele ya wanasimba wanazi.

Unapotoa taarifa rasmi ya klabu kupitia kwa Afisa habari aliyeita vyombo vya habari kuitangaza au kuitoa ni kwamba uongozi umeridhia jambo hilo kuanzia Sekretarieti ambayo iko chini ya Afisa Mtendaji Mkuu mpaka Bodi ya Wakurugenzi ambayo ipo chini ya Mwenyekiti wa Bodi.

Mnapoghairisha maamuzi ya mwanzo mnapaswa pia kutoa taarifa rasmi hata kwa Press release ili kujenga Taasisi inayofuata weledi kwenye kufanya kazi zake. Haiwezekani jezi iliyostaafishwa ikaonekana kiwanjani kwenye msimu huo huo tena kwenye mechi rasmi hatakama sio ya kimashindano.

Jezi namba 20 kama taarifa ya awali ilifutwa kwenye namba za jezi za wachezaji wa Senior team msimu huu, kuonekana tena kiwanjani bila maelezo ni ishara mbaya kwa uongozi wa Simba inayojinasibu kuendesha mambo kwa weledi huku hili linatokea bila taarifa rasmi.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here