Home KITAIFA MAYELE AIKATAA YANGA HADHARANI MBELE YA MASHABIKI, ASEMA YEYE SIO SHABIKI WA...

MAYELE AIKATAA YANGA HADHARANI MBELE YA MASHABIKI, ASEMA YEYE SIO SHABIKI WA YANGA, TIMU YAKE HII HAPA

0

Mshambuliaji wa zamani wa AS Vita Club ya Congo na Yanga SC, Fiston Kalala Mayele ambae kwa sasa nakipiga kwenye Klabu ya Pyramids FC ya Misri amekataa kuwa yeye si shabiki wa Yanga bali ni Shabiki wa As Vita.

Mayele ametoa majibu hayo baada ya shabiki wa Yanga @akili5000 kumchokonoa kwenye comment katika picha aliyospost mchezaji huyo kwa kuandika; “Shabiki mkubwa wa Yanga anaecheza Pyramid.”

Baada ya comment hiyo Mayele alijibu kwa kuandika; “Mimi ni Shabiki wa As Vita bana.”

Ikumbukwe kuwa Mayele alijiunga na Yanga msimu wa 2021/22 ambapo ameitumikia timu hiyo kwa miaka miwili mpaka mwishoni wa msimu ulipomalizika akiwa ameisaidia kushinda mataji sita ya ndani kwa miaka miwili, kufika fainali ya CAFCC na yeye mwenyewe kuibuka mfungaji bora wa Ligi Kuu ya NBC na mfungaji bora wa michuano ya CAFCC.

Yanga walihitaji zaidi kumbakisha Mkongomani huyo lakini Waarabu walimwaga mkwanja wa kutosha ambao ulimshawishi kuachana na mabosi zake hao wa Jangwani na kutimkia Misri hivi karibuni.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here