Home KITAIFA MIKWARA YA NGAO YA JAMII IMESHAANZA, BENO ATAMBA MBELE YA SIMBA

MIKWARA YA NGAO YA JAMII IMESHAANZA, BENO ATAMBA MBELE YA SIMBA

0
Beno Kakolanya

Mlinda Lango Beno Kakolanya amesema atahakikisha anafanya vizuri katika timu yake mpya ya Singida Fountain Gate, kama atapangwa kucheza katika mchezo wao wa Nusu Fainali ya Ngao ya Jamii dhidi ya Simba SC.

Akizungumza kuelekea mchezo huo utakaopigwa Agosti 10 katika Uwanja wa CCM Mkwakwani jijini Tanga, Kakolanya amesema atahakikisha anaonyesha kiwango bora na kuisaidia timu yake kupata matokeo mazuri.

“Najua Simba SC ina wachezaji wazuri kutokana na usajili iliyoufanya, lakini hata timu yetu ina kikosi kizuri mimi na wenzangu tutapambana kuhakikisha tupanata ushindi,” amesema.

Kakolanya anajua baada ya kusajiliwa Singida kibarua chake cha kwanza ni dhidi ya Simba SC aliyotoka, hivyo hatakubali kuona timu yake inapoteza katika mchezo huo.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here