Home KITAIFA MOSES PHIRI: NILIENDA KUTAFUTA MPIRA NILIOUKOSA JANA

MOSES PHIRI: NILIENDA KUTAFUTA MPIRA NILIOUKOSA JANA

0

Mshambuliaji wa Simba Moses Phiri ameandika katika mtandao wa Instagram kuwa amechelewa kuchapisha picha akiwa na Ngao ya Jamii kwakuwa alitingwa katika kuutafuta mpira uliopotea Usiku wa jana katika uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.

“Pole jamani nimechelewa kwa sababu nilienda kutafuta mpira nilioukosa jana. Firstly Thank you to all Simba fans who celebrated with us yesterday night good effort to all the players including the board members who came through asanteni” Ameandika Phiri.

Itakumbukwa mara baada ya kutamatika kwa dakika 90 ya fainali ya Ngao ya Jamii kwa matokeo ya Yanga 0-0 Simba, hatua iliyoamua kuelekea katika changamoto ya mikwaju ya penati ambapo Simba iliibuka ushindi wa penati 1-3.

Kwa matokeo hayo Simba imetawazwa kuwa bingwa mpya wa Ngao ya Jamii na kufikia rekodi ya Yanga ya kubeba taji hilo mara Saba.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here