Home KITAIFA MSUVA AMWAGA SIRI ZA KIPA MMOROCCO WA SIMBA HADHARANI

MSUVA AMWAGA SIRI ZA KIPA MMOROCCO WA SIMBA HADHARANI

0
msuva

Mshambuliaji wa Timu ya Taifa ya Tanzania, Simon Happygod Msuva ametoa onyo kwa timu za Ligi Kuu akisema kipa mpya wa Simba, Ayoub Lakred kutoka FAR Rabat ya Morocco ana kiwango bora sana uwanjani.

Simba walimtangaza kipa huyo wiki iliyopita akichukua nafasi ya Mbrazil, Luis Jefferson aliyedaiwa kupata majeraha kwenye kambi ya timu hiyo Uturuki kufuatia kipa wao namba moja, Aishi Salum Manula kuwa majeruhi ambayo yatamweka nje ya dimba kwa muda mrefu.

Msuva amesema wakati akiwa Wydad Casablanca ya nchini Morocco, aliwahi kukutana mara kadhaa na FAR Rabat na golini alikuwepo Lakred, hivyo anakumbuka kile kipa huyo alikifanya.

“Mara ya mwisho nilikuwa benchi na timu yetu iliifunga FAR Rabat bao 1-0, alionyesha kiwango kizuri ni kipa bora na watu wasishangae kama atachukua nafasi haraka Simba, miaka imeenda tangu kipindi hicho ambacho nilikuwa nikicheza Morocco kwa hiyo sijui kwa sasa kama atakuwa na ubora uleule au umeongezeka lakini kijumla anaweza kufanya mambo makubwa kwenye ligi na ana uzoefu wa kimataifa,” alisema.

Jumatatu ya Oktoba 5, 2021 katika mchezo wa raundi ya 15 kwenye ligi ya Morocco maarufu kama Batola Pro, Msuva alikuwa mmoja wa washambuliaji wa Wydad Casablanca ambao walichemka kumfunga Lakred ambaye aliisaidia FAR Rabat kuvuna pointi moja ikiwa nyumbani baada ya mechi kumalizika kwa suluhu.

Hata hivyo, katika lango la FAR Rabat walikuwa wakipishana kati ya nyota huyo wa sasa wa Simba na Mohamed Baayou ambaye kwa sasa hana timu.

Kwa mujibu wa Adrian Kitare ambaye yupo kwenye timu ya vijana wa Raja Casablanca, alimwelezea Lakred ni kipa mwenye uwezo mkubwa na uzoefu unaweza kuisaidia Simba kwenye michuano ya kimataifa.

“Namjua kwa sababu nimekuwa nikifuatilia ligi ya Morocco tangu niwe huku, ni mzuri kwenye mikwaju ya penalti pia, huwa anacheza mipira ya krosi na ni mwongeaji mzuri tu akiwa golini. Sijui kwa nini FAR iliachana naye lakini atakuwa nguzo muhimu Simba,” alisema Adrian.

Ayoub alizaliwa na kukulia huko Bouznika, Morocco na alijiunga na akademi ya RS Berkane akiwa na umri mdogo na sasa anaitumikia timu ya vijana ya Raja.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here