Home KITAIFA NYOTA MPYA YANGA AJA NA UJUMBE HUU

NYOTA MPYA YANGA AJA NA UJUMBE HUU

0
HAFIZ Konkoni mshambuliaji mpya wa Yanga amesema kuwa yupo tayari kwa ajili ya msimu mpya wa 2023/24.

HAFIZ Konkoni mshambuliaji mpya wa Yanga amesema kuwa yupo tayari kwa ajili ya msimu mpya wa 2023/24.

Nyota huyo anatajwa kuwa mbadala wa mshambuliaji Fiston Mayele ambaye amesepa Yanga na kuelekea kupata changamoto mpya ndani ya Pyramids ya Misri.

Mayele ameweka wazi kuwa anaamini wachezaji wapya ambao wapo ndani ya kikosi cha Yanga pamoja na wale ambao walikuwa pamoja msimu wa 2022/23 watafanya vizuri.

Mshambuliaji huyo mpya raia wa Ghana amesema: “Natambua ushindani ni mkubwa lakini tutashirikiana na wachezaji wengine kupata matokeo tupo tayari.

“Kikubwa ni kufanya vizuri kwenye mechi zetu ambazo tunacheza na tunaamini kwamba kila kitu kitakuwa sawa hivyo mashabiki wazidi kuwa pamoja nasi,”.

Yanga inatarajiwa kucheza mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Azam FC, Uwanja wa Mkwakwani, Tanga Agosti 9.

Ikumbukwe kwamba ni timu nne zinashiriki msimu huu ikiwa ni Yanga yenyewe ambao walitwaa taji hilo msimu wa 2022/23 mbele ya Simba ambao nao wanashiriki pia, Singida Fountain Gate na Azam FC.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here