Home MAGAZETI LEO ORODHA YA MAKOCHA BONGO WASIOKIDHI VIGEZO, SIMBA, YANGA NDANI

ORODHA YA MAKOCHA BONGO WASIOKIDHI VIGEZO, SIMBA, YANGA NDANI

0
habari za michezo

KATIKA orodha ya makocha ambao hawajakidhi vigezo vya kukaa benchi katika mechi za Ligi Kuu Bara wapo pia makocha kutoka timu zilizomaliza nafasi tatu za juu.

Timu hizo ni Yanga, Simba na Azam FC ambazo zote zitashiriki mashindano ya kimataifa.

Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF), Agosti 15 lilitoa orodha ya makocha ambao hawajakidhi vigezo vya kukaa benchi katika mechi za ligi.

Kwa upande wa Yanga ni Kocha Msaidizi Moussa Ndaw ametajwa kuwa vigezo vyake havijatimia kuwa kocha msaidizi huku kwa upande wa Simba kocha wao msaidizi Ounnane Sellami naye hajakidhi vigezo.

Azam FC wao ni Yusuph Dabo na Khalifa Ababacar Fall wote wanashindwa kuwa na vigezo vya kufundisha katika Ligi Kuu Tanzania.

Mwinyi Zahera wa Coastal Union naye ni miongoni mwao ambapo wote hawana Leseni ya CAF Diploma A ambayo ndio kigezo kikubwa cha kuwa kocha Mkuu na msaidizi Bongo.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here