Home KITAIFA PAMOJA NA KUSHINDA NGAO YA JAMII, SIMBA WAPEWA ONYO SAFARI YA MOROGORO

PAMOJA NA KUSHINDA NGAO YA JAMII, SIMBA WAPEWA ONYO SAFARI YA MOROGORO

0

Uongozi wa Klabu ya Mtibwa Sugar, umebainisha kuwa, timu yao kwa sasa inaendelea na maandalizi ya msimu mpya ikiwa tayari kwa mechi zote zinazowahusu.

Timu hiyo inatumia Uwanja wa Manungu uliopo Morogoro kwa mechi za nyumbani, itaanza msimu wa 2023/24 kwa kupambana na Simba SC, ikiwa ni mechi ya Ligi Kuu Bara itakayochezwa Agosti 17.

Afisa Habari wa Mtibwa Sugar Thobias Kifaru, amesema, wapo tayari kwa ajili ya msimu mpya na wana imani ya watafanya vizuri.

“Tupo tayari kwa mechi zote ambazo tutacheza, hatuhofii ndio maana tupo kwenye ligi, sio Young Africans, Simba SC au Azam FC.”

“Tunatambua lazima tucheze na timu zote. Wapinzani wetu tunawaheshimu nasi tunafanya maandalizi kupata matokeo mazuri. Makosa ambayo yalifanyika msimu wa 2022/23 hayo benchi la ufundi linayafanyi kazi” amesema Kifaru.”

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here