Home KIMATAIFA PAMOJA NA UWEPO WA SIMBA NA YANGA, HUYU HAPA MTZ ALIYEKULA SHAVU...

PAMOJA NA UWEPO WA SIMBA NA YANGA, HUYU HAPA MTZ ALIYEKULA SHAVU TIMU YA SAUZI

0
Ligi Kuu Bara

BAADA ya kufanya vizuri kwenye Ligi Kuu Bara akiwa na wakusanya mapato wa Kinondoni, KMC, kiungo wa boli wa Kitanzania, Baraka Majogoro amejiunga na Chippa United inayoshiriki Ligi Kuu ya Afrika Kusini na ni miongoni mwa waliosajiliwa msimu huu wakibeba matumaini ya timu hiyo msimu huu.

Chippa ambayo ilijinasua kwenye janga la kushuka daraja msimu uliopita, kwenye mitandao yao wa kijamii walimtambulisha Majogoro na inadaiwani chaguo la kocha wa kikosi hicho, Morgan Mammila.

Mammila ameonakana kutaka kukiongezea nguvu kikosi chake katika maeneo tofauti ikiwemo eneo la kiungo mkabaji na Majogoro amekuwa akimudu kucheza tangu akiwa na Mtibwa Sugar kabla ya kutua KMC.

Majogoro amepokewa vizuri na mashabiki wa timu hiyo wakiamini atafanya vizuri. Timu hiyo aliiwahi kuichezea Mtanzania Abdi Banda ambaye amejiunga na Richards Bay ya ya ligi hiyo kwa mkataba wa mwaka mmoja.

Mammila ambaye jana, Jumapili alikuwa na kibarua cha kuiongoza Chippa United kucheza mchezo wao wa kwanza wa msimu kwenye ligi dhidi ya Kaizer Chiefs, anaamini maingizo waliyoyafanya yatakuwa na matunda kutokana na namna walivyowafuatilia wachezaji hao.

“Wameonyesha ni wachezaji wazuri na wakomavu wanaoweza kuongeza ubora wa kikosi chetu, yapo mapungufu machache tuliyoyaona, hivyo kilichobaki ni kupambana na kuona kwa namna gani tunaweza kufikia malengo yetu msimu huu,” anasema na kuongeza;

“Ni kiungo mzuri (Majogoro) mwenye uwezo wa kuzuia na kuchezesha timu, ni kitu tulichokuwa tunakihitaji na kwa kushirikiana na wachezaji wenzake naamini tutafanya kile tulichodhamiria.”

Mbali na Majogoro wachezaji wengine waliosajiliwa na Chippa United ni Andile Fakude, Thabang Maloa, Senzo Nkwanyana na Lukhanyo July.

Majogoro anasema hii ni nafasi kubwa na anaamini ataitumia vizuri kuhakikisha anaonyesha kipaji chake.

“Ni changamoto mpya katika maisha yangu ya soka. Namshukuru Mungu kwa haya yote na ninatarajia kuwafurahisha wapenzi wa soka na mashabiki wa Chippa United,” anasema kiungo huyo.

Nahodha wa Taifa Stars, Mbwana Samatta ambaye katika dirisha hili ajiunga na PAOK ya Ugiriki akitokea Fenerbahce ya Uturuki ni miongoni mwa waliompongeza Majogoro huku akimtaka kukaza buti ili kuendelea kuipeperusha Bendera ya Tanzania nchini humo.

Majogoro ni mchezaji wa pili wa Kitanzania kutoka Ligi Kuu Bara kutua Afrika Kusini katika dirisha hili la usajili baada ya Abdul Mohamed aliyejiunga na Supersport United akitokea Mbeya City.

HII NDIO CHIPPA

Klabu hii ilianzishwa Januari 2010 wakati Chippa Mpengesi alipoinunua Mbekweni Cosmos. Cosmos ilikuwa imepanda daraja kutoka Ligi ya Castle mwishoni mwa msimu wa 2008-09. Katika msimu wa 2010-11, klabu ilianza kucheza chini ya jina, Chippa United.

Msimu wa kwanza wa Chippa United ulikuwa wa mafanikio sana kwa klabu hiyo kushinda Ligi ya Vodacom ya Western Cape kabla ya kushinda Ligi ya Vodacom ya Kitaifa, Coastal Stream na kupandishwa daraja hadi Daraja la Kwanza la Kitaifa.

Chippa pia ilitawazwa mabingwa wa jumla wa Ligi ya Vodacom 2010-11 baada ya kuwashinda washindi wa Inland Stream Sivutsa Stars.

Klabu hii ilimaliza msimu wao wa kwanza katika Ligi ya Taifa ya Daraja la Kwanza nafasi ya pili nyuma ya Chuo Kikuu cha Pretoria na ikashinda kupanda hadi Ligi Kuu kupitia mechi za mchujo mwezi Juni 2012.

Chippa United inamilikiwa kikamilifu na Chippa Investment Holdings, ambayo ni kampuni ya ujenzi, ulinzi na usafi ya mjini Cape Town iliyoanzishwa na Siviwe ‘Chippa’ Mpengesi.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here