Home KITAIFA RAIS SAMIA MGENI RASMI SIMBA DAY

RAIS SAMIA MGENI RASMI SIMBA DAY

0
Simba Day

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi Simba Day.

Tukio hilo la kutambulisha wachezaji pamoja na benchi la ufundi linatarajiwa kufanyika Uwanja wa Mkapa, Agosti 6 2023.

Tayari Simba imetambulisha msanii mkubwa Afrika Mashariki, Ali Kiba ambaye aliwahi kuwa shabiki wa Yanga na sasa amehamia Simba huyu atakuwa kiongozi wa watumbuizaji siku hiyo.

Katika tamasha la Yanga wasanii mbalimbali walipanda jukwaani kutoa burudani ikiwa ni pamoja na Jux wa asante.

Mama anatarajiwa kuwa miongoni mwa wageni wa heshima akiwa ni mgeni rasmi atakayeshuhudia utambulisho wa wachezaji pamoja na benchi la ufundi.

Taarifa kutoka Simba zimeeleza kuwa wanatanguliza shukrani kwa rais kuridhia ombi la kuwa mgeni rasmi kwenye tukio kubwa.

Tayari Yanga watani za jadi wa Simba wamekamilisha tukio lao la utambulisho ambapo walicheza dhidi ya Kaizer Chiefs mchezo wa kirafiki wakashinda bao 1-0.

Bao la Yanga lilifungwa na Kennedy Musonda kisha Singida Fountain Gate ilikuwa ni Singida Big Day walipata ushindi wa mabao 2-1 AS Vita .

Agosti 6 ni Simba Day, Uwanja wa Mkapa pia Simba wametangaza tiketi zote kununuliwa.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here