Home KITAIFA SIMBA KUMSAJILI KIPA HUYU KUTOKA KWA NABI

SIMBA KUMSAJILI KIPA HUYU KUTOKA KWA NABI

0

Simba imefikia makubaliano ya kuinasa saini ya kipa, Ayoub Lakred (28) aliyekuwa akiichezea timu ya FAR Rabat ya Morocco inayofundishwa na kocha wa zamani wa Yanga, Nasreddine Nabi.

Chanzo makini kutoka ndani ya timu hiyo kimesema makubaliano hayo yamefikiwa ikiwa ni siku chache tangu kuachana na Mbrazili, Jefferson Luis aliyeondolewa kambini nchini Uturuki kutokana na majeraha ya misuli..

“Ni kweli yupo nchini na maongezi hadi sasa yanaendelea vizuri, ni matumaini yetu atakuwa msaada mkubwa kutokana na ushiriki wetu wa mashindano mengi ya ndani na kimataifa,” kilisema chanzo changu.

Usajili wa Lakred unakuwa ni wa pili kwa kipa ndani ya kikosi hicho. Lakred aliyezaliwa Juni 1995, alichezea FAR Rabat, timu nyingine aliyowahi kuichezea ni RS Berkane.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here