Home KITAIFA WADAU WAITABIRIA YANGA KUNYAKUA NGAO YA JAMII ISHU IKO HIVI

WADAU WAITABIRIA YANGA KUNYAKUA NGAO YA JAMII ISHU IKO HIVI

0
Ngao Ya Jamii

Baadhi ya wachambuzi wa soka na wadau wa kabumbu nchini wanaipa Young Africans Sports zaidi ya asilimia 50 kushinda taji la Ngao ya Jamii mbele ya mtani wake Simba SC huku wakitoa sababu mbalimbali.

Miongoni mwa sababu ikiwa ni pamoja na muunganiko mzuri uliyopo ndani ya kikosi cha Yanga, wakati Simba wakionekana bado wanajitafuta ili kuupata muunganiko.

Pili matokeo kwenye mechi zao za hivi karibuni ikiwemo zile za utambulisho wa wachezaji na hizi mbili za mwisho za Nusu Fainali ya Ngao ya Jamii.

Yanga SC wameonekana imara zaidi hata kupelekea kushinda goli 2-0 dhidi ya Azam FC, wakati Simba SC akilazimishwa sare tasa ya 0-0 mbele ya Singida Fountain Gate FC mpaka kupelekea kupigwa mikwaju ya penati.

Kwenye mitandao ya kijamii ya Instagram ya timu hizi Yanga SC wapo ‘serious‘ na mazoezi wakati Simba SC bado wana Furaha ya Kutinga Fainali kwa kumfunga Singida kwa mikwaju ya penati (4-2).

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here