Home KITAIFA WINGA WA YANGA AONA ISIWE TABU AMFUATA NABI FAR RIBAT

WINGA WA YANGA AONA ISIWE TABU AMFUATA NABI FAR RIBAT

0

ALIYEKUWA winga wa Yanga, Bernard Morrison yupo nchini Morocco na taarifa za uhakika ni kwamba anafukuzia dili la kuwatumikia mabingwa wa nchi hiyo FAR Rabat.

FAR Rabat ambayo sasa inafundishwa na kocha wa zamani wa Yanga Nasreddine Nabi inapiga hesabu za kumchukua Morrison wakiwa kwenye msako wa kusaka winga kulingana na mahitaji ya kocha huyo mpya ambaye hatahivyo awali akiwa nae Jangwani alikuwa hamkubali kiviile.

Taarifa za ndani kutoka kwa mtu wa karibu na Morisson zimeliambia Mwanaspoti kuwa mchezaji huyo raia wa Ghana yupo nchini humo na kama mambo yataenda sawa atasaini miaka miwili.

Mbali na majaribio hayo pia winga huyo huenda akapewa mkataba mgumu kutokana na Nabi tayari ana faili lake la jinsi alivyoishi naye ndani ya Yanga.

FAR Rabat inasaka mawinga wawili wa kulia na kushoto katika kuboresha kikosi hicho ambacho msimu ujao kitashiriki Ligi ya Mabingwa Afrika.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here