Home KITAIFA YANGA :- SIMBA WAMEMKOSEA HESHIMA MANGUNGU….KWA NINI HAKUKAA NA RAIS SAMIA..?

YANGA :- SIMBA WAMEMKOSEA HESHIMA MANGUNGU….KWA NINI HAKUKAA NA RAIS SAMIA..?

0
Simba

Jumapili iliyopita Simba walikuwa na Tamasha lao la “Simba Day” katika Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.

Kilele cha Tamasha hilo kilifana sana huku Simba wakipongezwa na wadau mbalimbali wa soak kwa namna walivyofanikisha Tamasha hilo.

Mgeni Rasmi katika Tamsha hilo alikuwa ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.

Miongoni wa watu waliotoa pongezi zao ni Mkurugenzi wa Sheria wa Yanga wakili Simon Patrick ambae kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika;

Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan alinogesha sherehe yenu watani hongereni, ila siku nyingine rekebisheni protocol, Mwenyekiti wa Klabu Mzee Mangungu sio wa kukaa VIP A, alipashwa akae hapo na mgeni rasmi kwani yeye ndio Kiongozi wa juu kwenye Klabu.

Je unakubaliana na kauli na ushauri huo wa Wakili Simon Patrick? Tupe maoni yako

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here