Home KITAIFA AL MARREIKH TUMBO JOTO,GAMONDI AMVURUGA KOCHA WAO

AL MARREIKH TUMBO JOTO,GAMONDI AMVURUGA KOCHA WAO

0
Gamondi

Kocha Mkuu wa Al Merrikh ya Sudan, Osama Nabieh ameweka wazi kuhofia ubora wa wachezaji wa Young Africans wanaongozwa na viungo Pacome Zouzoua na Maxi Mpia, huku akisema anatarajia kukutana na mtihani mzito mbele ya Mabingwa hao wa Tanzania Bara kutokana na ubora wao walionao.

Akizungumza kutoka Kigali Rwanda kocha huyo amesema: “Tunatarajia kukutana na upinzani mgumu kutoka kwa Young Africans kutokana na ubora wao mkubwa ambao wamekuwa wakiuonyesha katika michuano ya kimataifa siku za karibuni.

“Wanao wachezaji wazuri ambao nimewaona na tayari wachezaji wangu wanafahamu cha kufanya kutokana na maelezo ambayo nimewapa.

“Malengo yetu ni kuona tunafika makundi kama msimu uliopita, sisi tunayo changamoto ya kukosa mechi nyingi lakini naamini tunayo nafasi nzuri ya kuendelea kufanya vyema dhidi yao na kutimiza malengo yetu.

“Tumepata muda mzuri wa kujiandaa na sasa kilichobaki ni kuwa tayari kwa ajili ya mchezo wetu wa kwanza tukiwa nyumbani,” amesema kocha huyo.

Kwa upande wa kocha wa Young Africans, Miguel Gamondi akizungumzia mchezo huo amesema; Tupo katika maandalizi ya nguvu kuhakikisha mashabiki wetu wanaendelea kupata furaha ya ushindi.

“Naendelea kuboresha baadhi ya maeneo ambayo nimeona ni muhimu katika kikosi changu ili kuhakikisha tunapata mabao mengi kwenye michezo ijayo ukiwemo dhidi ya Al Merrikh,” amesema Gamondi.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here