Home KIMATAIFA ALIYEKUWA MMILIKI WA FULHAM AFARIKI DUNIA

ALIYEKUWA MMILIKI WA FULHAM AFARIKI DUNIA

0

Aliyekuwa mmiliki wa klabu ya soka ya Fulham na duka kuu la Harrods huko London Mohamed al-Fayed amefariki dunia katika Jiji la London, Uingereza.

Taarifa kutoka katika familia ya bilionea huyo inaeleza kuwa Al-Fayed, alizaliwa nchini Misri na amefariki akiwa na umri wa miaka 94.

“Bi Mohamed al-Fayed, watoto wake na wajukuu wangependa kuthibitisha kwamba mume wake mpendwa, baba yao na babu yao, Mohamed, amefariki dunia kwa amani siku ya Jumatano Agosti 30, 2023,” familia yake ilisema katika taarifa iliyotolewa na klabu ya soka ya Fulham Ijumaa.

“Alifurahia kustaafu kwa muda mrefu na kufariki akiwa amezungukwa na wapendwa wake. Familia imeomba faragha yao iheshimiwe wakati huu.” familia hiyo ilisema.

Al-Fayed anakumbukwa kama baba wa Dodi Fayed mpenzi wa zamani wa Princess Diana wa Uingereza waliofariki pamoja katika ajali ya gari huko Paris, Ufaransa mnamo 1997.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here