Home KITAIFA ALLY KAMWE ATAMBA NA UBORA WA YANGA KIMATAIFA

ALLY KAMWE ATAMBA NA UBORA WA YANGA KIMATAIFA

0
ali kamwe

Ally Shaban Kamwe ambaye ni Afisa Habari wa Yanga Africans, ametamba kuwa, wao ndio wawakilishi pekee wa Kimataifa wenye uhakika wa kufanya vizuri kwenye mashindano ya Klabu Bingwa Afrika.

Kamwe ameyasema hayo leo Septemba 12, 2023 alipokuwa akifanya mahojiano na Wasafi Media kuhusu mipango yao kuelekea mchezo wao wa hatua ya kwanza dhidi ya Al Merrikh.

“Tunaweza kuwa tupo wengi darasani lakini sisi pekee ndio tuna uhakika wa kufanya vizuri kwenye michuano ya Klabu Bingwa Afrika,” alisema Ally.

Msemaji huyo alisema anatamka hivyo mapema kwani kila kitu kimejidhihirisha mapema kabisa, Yanga wameanza kutwaa tuzo za mwezi Agosti ambapo kocha bora na mchezaji bora ametokea kwenye kikosi chao.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here