Home KITAIFA DUCHU, SASA NI ZAMU YAKE NA ISRAEL HUYU ZIMBWE, KAPOMBE WAPUMZISHWE SASA

DUCHU, SASA NI ZAMU YAKE NA ISRAEL HUYU ZIMBWE, KAPOMBE WAPUMZISHWE SASA

0
simba

Kocha Jamhuri Kihwelu Julio amesema kuwa, mabeki wa pembeni wa Simba SC, Mohamed Hussein ‘Zimbwe Jr’ na Shomari Kapombe wamechoka kwa kutumika muda mrefu, hivyo waachie damu changa ili ziweze kuendeleza pale walipofikia.

Julio amesema hayo mara baada ya mjadala mkubwa kuibuka kuwa mabeki hao wametumika ndani ya Simba na timu ya Taifa ya Tanzania kwa miaka mingi hali inayopelekea kuchoka na sasa kushindwa kutimiza vyema majukumu yao.

“Zimbwe na Kapombe ni vijana wangu,ni wachezaji bora sana lakini kwa sasa wamechoka sana lazima niseme ukweli, wapo vijana kama Israel Mwenda na David Kameta Duchu wana uwezo mkubwa sana ndio maana wamesajiliwa kwa fedha nyingi lakini hawapewi nafasi, mimi ninaamini wakipewa nafasi watawasaidia sana hawa wachezaji.

“Hata kwenye masuala ya utawala, Hayati Mwalimu Nyerere angeamua kutawala miaka yote basi tusingemuona Mzee Mwinyi, Hayati Mkapa, Dkt. Kikwete, Hayati Magufuli na sasa Dkt. Samia, lazima turuhusu kutoa nafasi kwa vijana wenye vipaji watasaidia maendeleo lakini tusipobadilika tutapiga kelele kila siku.

“Huko Ulaya tunaona wenzetu wanaruhusu vijana kucheza tena wakiwa na umri wa miaka 18, huku kwetu tunataka kufanikiwa na wachezaji wenye umri mkubwa haiwezekani,” amesems Jamhuri Kihwelu Julio akizungumza na David Kampista.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here