Wakati Yanga ikiibuka na ushindi wa mabao 2-0 ugenini, Watani zao Simba SC walilazimishwa sare ya Mabao 2-2 dhidi ya Power Dynamos kutoka Zambia katika Uwanja wa Levy Mwanawasa.
Sasa mchambuzi wa michezo kutoa kituo cha redio cha EFM. Jemedari Said amesetoa maoni yake kuhusiana na sare hiyo.
Akizungumza Jemedari Said amesema;
“Simba wana wachezaji wengi bora kimbinu, lakini hawajitumi. Yanga ukiwaangalia wanavyocheza wakiwa hawana mpira,ni tofauti wanavyocheza Simba wakiwa hawana mpira. Simba ni wavivu,”
“Wanawapa (wapinzani) muda mwingi wa kuwa na mpira. Nafasi hiyo (mpinzani) hawezi kuipata kwa Yanga kwa sababu anakuwa kwenye Presha, anakabwa.”
“Yanga kwani timu yao inakaba vizuri na hawatoi muda na nafasi kwa mpinzani anapokuwa na mpira.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE