Home KIMATAIFA MAKUBWA: HAT-TRICK YA “KANE” IMEFUTWA, KISA KIZIMA HIKI HAPA

MAKUBWA: HAT-TRICK YA “KANE” IMEFUTWA, KISA KIZIMA HIKI HAPA

0
Harry Kane

Nyota wa Bayern Munich Harry Kane alifunga hat-trick yake ya kwanza Bundesliga kwa Bayern Munich, lakini haikuhesabiwa kutokana na sheria za soka Ujerumani.

Nahodha huyo wa kimataifa wa England aliisaidia Bayern kufunga mabao matatu katika ushindi wa mabao 7-0 dhidi ya Vfl Bochum kwenye Uwanja wa Allianz Arena huku ikidhaniwa kuwa alifunga hat trick.

Kane alifunga bao lake la kwanza katika dakika ya 12 kisha akaongeza mabao yake mawili kipindi cha pili. Hata hivyo, hat-trick hiyo haikuhesabiwa kwa sababu tayari kuna mchezaji alishafunga bao katikati ya mabao mawili aliyofunga Kane.

Hiyo ina maana kwamba Kane alitakiwa kufunga mabao matatu mfululizo bila ya mchezaji mwingine kufunga katikati ya mabao hayo.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here