Home KITAIFA MANULA KUANZA NA WAARABU, DAKTARI AFUNGUKA

MANULA KUANZA NA WAARABU, DAKTARI AFUNGUKA

0
manula

Timu ya Simba haijapoteza mchezo wowote msimu huu hadi sasa na inawezekana mambo yakawa mazuri zaidi baada ya kipa wao namba moja Aishi Manula kurejea uwanjani baada ya daktari kusema bado wiki tatu.

Manula alikuwa nje ya uwanja tangu mwisho mwa msimu uliopita baada ya kuumia nyama za paja, lakini sasa daktari wa timu hiyo, Edwin Kagabo amesema anahitaji wiki tatu tu kuungana na wenzake uwanjani, hali ambayo inaonyesha anaweza kuiwahi mechi ya ufunguzi wa michuano mipya ya African Football League (AFL) dhidi ya mabingwa mara 10 wa Afrika, Al Ahly ya Misri, Kwa Mkapa, Oktoba 20.

Simba inatakiwa kuwa na kikosi imara kutokana na kuwa na majukumu mazito msimu huu ikishiriki michuano sita tofauti ukianza na Ngao ya Jamii, Ligi Kuu Bara, Ligi ya Mabingwa Afrika, Kombe la Mapinduzi, Kombe la ASFC na michuano mipya ya AFL ambayo awali iliitwa Super League.

Manula pamoja na kuanza mazoezi mepesi ya uwanjani na wenzake lakini tangu Julai alikuwa ameanza mazoezi binafsi ya gym huku akionekana kurejea haraka kuliko matarajio.

“Sio kwamba makipa waliopo hawana uwezo wa kudaka, lakini Manula kwa mujibu wa wataalamu wetu ni kuwa anaendelea vizuri na anaweza kudaka mechi dhidi ya Al Ahly ingawa bado tutakuwa tukifanya mawasiliano na daktari kujua maendeleo yake ya kila siku”. amesema.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here