Home KITAIFA MANULA YUPO TAYARI KUTOA BURUDANI

MANULA YUPO TAYARI KUTOA BURUDANI

0

DAR ES SALAAM: Afya ya mlinda lango wa Simba na timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’, Aishi Manula ‘Tanzania One’ inaelezwa kuimarika.

Hii ni kwa mujibu wa picha mnato zilizorushwa na mitandao rasmi ya kijamii ya klabu yake.

“Air Manula ndani ya Mo Simba Arena kwa mara ya kwanza tangu alipopata majeraha” Simba imedokeza, na kuamsha matumaini kwa wana Simba juu ya kurejea kwa Mlinda lango huyo.

Itakumbukwa, taarifa iliyochapishwa na tovuti ya Simba mnamo Mei 29, 2023 ilidokeza kuwa Tanzania One amesafiri kwenda Afrika Kusini kwaajili ya matibabu ya nyama za paja.

Hali iliyomfanya Manula kukosa michezo ya mwisho ya msimu wa 2022/23 sambamba na mechi za michuano ya Ligi ya Mabingwa barani Afrika (CAFCL).

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here