Home KITAIFA MAXI AMTAJA MAYELE KWENYE KIKSOSI CHA YANGA TAMAA YAKE IKO HIVI

MAXI AMTAJA MAYELE KWENYE KIKSOSI CHA YANGA TAMAA YAKE IKO HIVI

0
mayele

Kiungo wa Yanga, Maxi Mpia Nzengeli ameweka wazi kutamani kucheza na Fiston Mayele katika kikosi cha Yanga tofauti na alivyoondoka.

Maxi Nzengeli wakati anasajiliwa Yanga alimkuta mshambuliaji huyo akiwa kwenye hatua za mwisho za kujiunga na klabu ya Pyramid FC ya Misri.

Maxi Nzengeli alisema kuwa alitamani kucheza na Mayele katika kikosi cha Yanga kwani anaamini angemfanya azidi kufunga mabao mengi huku akisema kuwa anamtakia kila la heri huko alipoenda.

“Nilitamani kucheza na Mayele ndani ya Yanga, wakati nafahamu kuwa naenda kujiunga na Yanga niliwaza kuwa nitaenda kucheza na Mayele na nitamsaidia kufanya vizuri zaidi.

“Niliamini kuwa kwa ubora wangu na wake tungeifanya Yanga kuwa bora zaidi, mimi niseme tu nimtakie kila la heri alipoenda. Sisi kwa sasa tutaipambania Yanga ili izidi kuwa bora zaidi,” alisema mchezaji huyo.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here