Home KITAIFA MAXI AWEKA WAZI HESABU HIZI ZA YANGA KWA AL MAREIKH

MAXI AWEKA WAZI HESABU HIZI ZA YANGA KWA AL MAREIKH

0
maxi

Kiungo mshambuliaji wa Klabu ya Yanga, Maxi Ngzengeli amesema kuwa hesabu zao ni kushinda ugenini dhidi ya Al-Merrikh ya Sudan ugenini nchini Rwanda kabla hawajacheza mchezo wa marudiano.

Nzengeli ambaye ametua Jangwani msimu huu akitokea AS Maniema Union ya DR Congo na kuonyesha uwezo mkubwa, amekuwa tegemo ndani ya klabu hiyo katika mechi chache alizocheza tangu ajiunge na Wananchi.

Yanga ambao tayari wamewasili Rwanda, wataingia katika Dimba la Pele, Kigali kesho Jumamosi, Septemba 16, 2023 kuvaana na Merrikh kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Barani Afrika.

“Tunakwenda Rwanda kucheza mechi ngumu ambayo malengo yetu ni kuhakikimsha tunashinda hukohuko. Hesabu zetu ni kushinda kule ugenini ili tukirudi hapa tumalizie kazi kuipeleka timu yetu hatua ya makundi kila mchezaji anatamani hii mechi,”

“Tumeona video za mashabiki wetu wanaokwenda imetupa nguvu sana na kujiona kuna kitu kikubwa tunatakiwa kukifanya kuwapa furaha ya ushindi,” amesema Maxi Nzengeli.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here