KOCHA Mkuu wa Kagera Sugar, Mecky Maxime amefichua kuwa kwa sasa kikosi chake kinaendelea na mazoezi ikiwa ni baada ya kuanza vibaya kwenye michezo yao ya Ligi Kuu Bara.
Baada ya kucheza mechi mbili haijakusanya pointi huku vinara wakiwa ni Yanga wenye pointi sita kibindoi.
Kagera imeanza vibaya katika ligi baada ya kupoteza mechi zake dhidi ya Mashujaa FC kwa mabao 2-0 na Ihefu 1-0.
Maxime amesema: “Ni kweli tumeanza vibaya Ligi Kuu Bara nimewahimiza wachezaji wangu na kuwaambia waongeze umakini wakiwa uwanjani.
“Maandalizi yanaendelea vizuri na Kila mchezaji ana morali na kile ambacho tunafanya mazoezini.
“Nawaandaa wachezaji kiakili na kuwapa fitinesi kwa ajili ya kujihakikishia wanapambana na kushinda mechi zote na kujiweka kwenye nafasi nzuri.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE