Home KITAIFA MUDATHIR AWEKA SIRI ZA GAMONDI HADHARANI

MUDATHIR AWEKA SIRI ZA GAMONDI HADHARANI

0
gamondi

KIUNGO wa Yanga, Mudathir Yahya amefichukua sababu kubwa iliyopelekea afunge bao pekee katika mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Namungo ni kutokana na kufuata maelekezo ya kocha wake Miguel Gamondi kabla ya kuingia uwanjani.

Kiungo huyo ametoa kauli hiyo kufuatia ushindi wa bao pekee alilofunga katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliopigwa juzi Jumatano kwenye Uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi, Dar.

Akizungumza na Championi Ijumaa, Mudathir alisema kuwa awali walitengeneza nafasi nyingi na kushindwa kuzitumia kabla ya Gamondi alipomnyanyua na kumuambia kuwa anahitaji kwenda kusahihisha makosa ili waweze kupata ushindi.

Kiungo huyo aliongeza kuwa, alifanikiwa kufanyia kazi majukumu aliyopewa na kocha huyo na kufanikiwa kufunga bao la ushindi dakika ya 88 akiunganisha krosi nzuri ya Yao Kouassi.

“Ni kweli kocha aliniambia nikafanye majukumu aliyonipa na kweli nimefanikisha kufanya hilo na kufunga bao pekee la ushindi na kurejea kileleni mwa msimamo wa ligi kuu.

“Tunawakikishia siku ya Septemba 30, waje kwa wingi katika mchezo wetu wa marudiano dhidi ya El Merrikh tutapambana kuhakikisha tunaenda kufuzu kucheza hatua ya makundi,” alisema kiungo huyo.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here