Home KITAIFA PACHA YA BALEKE, KRANO NA ONANA YAMFANYA MBRAZILI SIMBA KUJA NA HILI...

PACHA YA BALEKE, KRANO NA ONANA YAMFANYA MBRAZILI SIMBA KUJA NA HILI JIPYA

0
BALEKE SIMBA simba

BAADA ya michezo mitatu ya kirafiki kocha Mkuu wa timu Simba, Roberto Oliveira ‘Robertinho ameridhishwa na safu yake ya ushambuliaji kwa kila mchezaji anayecheza nafasi hiyo kufanyia kazi kile alichowaelekeza.

Katika michezo hiyo mitatu Jean Baleke, Willy Essomba Onana na Aubin Kramo waliweza kufanya vizuri na kufunga katika mechi zote tatu ikiwemo mechi ya leo Simba ilipocheza na kushinda mabao 6-0 dhidi ya Ngome FC.

Simba leo ilicheza mechi yake ya mwisho ya Uwanja wa Mo Arena Dar es Salaam hivyo kukamilisha michezo mitatu ya kirafiki kabla ya kuelekea nchini Zambia katika mchezo wao wa hatua ya pili ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Power Dynamos.

Katika mchezo huo wa juzi Simba iliendeleza kupata ushundi wa mabao 6 -0 yalifungwa na Shomari Kapombe, dakika ya 31, Kramo akiongeza la pili dakika ya 41 naye Jean Baleke alifunga bao la tatu dakika ya 45.

Simba aliongeza bao la nne dakika ya 66 kwa mkwaju wa penati baada ya Willy Essomba Onana kuchezewa madhambi ndani ya 18, Baleke alifunga bao la tano dakika ya 87 baada ya kumzidi ujanja mlinzi wa Kati wa Ngome, Shaban Chilunda alikamilisha karamu ya mabao dakika ya 89 baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa Mohamed Mussa.

Baada ya mechi hiyo leo Mo Simba Arena, Robertinho alisema kwenye mechi tatu walizocheza washambuliaji wote wamefanikiwa kufunga mabao jambo linalompa matumaini makubwa kwenye mchezo ujao wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Power Dynamos.

“Mchezo ulikuwa mzuri nimefurahishwa na kiwango cha wachezaji wangu kwa kupata ushindi katika michezo yetu mitatu.Huu utakuwa mchezo wa mwisho wa kirafiki rasmi tunaingia kwenye mipango ya kuikabili Power Dynamos kwenye mchezo wetu wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika,” alisema Robertinho.

Alisema kuwa michezo mitatu waliyocheza dhidi ya Kipanga , Cosmopolitan na Ngome FC imeongeza kitu kwenye maandalizi ya mchezo dhidi ya Power Dynamos, kwani wachezaji wote wamepata nafasi ya kucheza na kuweka miili sawa.

“Tumebakiza wiki moja kabla ya kuwavaa Power Dynamos hivyo tunahitaji wachezaji wote kuwa timamu na tayari tumepata kwenye michezo hii mitatu tuliyoianza, ” alisema Robertinho.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here