Home KIMATAIFA POGBA NA SAKATA JIPYA LA UTUMIAJI WA DAWA

POGBA NA SAKATA JIPYA LA UTUMIAJI WA DAWA

0
pogba

Kiungo wa Kimataifa wa Ufaransa Paul Pogba, amesimamishwa kusakata soka na Mamlaka ya kudhibiti matumizi ya dawa za kuongeza nguvu michezoni nchini Italia.

Uchunguzi huo uliomtia Pogba kwenye sakata hilo ulifanyika Agosti 20, 2023 kwenye mchezo wa Juventus dhidi ya Udinese

Huu ni Mkasa wa mwingine kwa Pogba baada ya hapo awali kiungo huyo kujikuta kwenye sintofahamu na ndugu zake huku kila upande ukimshtumu mwenzie hali iliyopelekea kuzorota kwa uhusiano wa familia yao.

pogba

Mkasa mwingine ni wa nyota huyo kushuhudia klabu yake ya Juventus ikizuiliwa kushiriki michuano ya Ulaya

Pogba bado mikasa imeendelea kumuandama kwani amekuwa akisumbuliwa na majeraha yaliyomfanya kushindwa kuitumikia timu yake kwa asilimia 100 tangu alipojiunga na timu hiyo mwaka 2022 akitokea Manchester United.

Ameichezea timu hiyo michezo nane tu ya ligi,huku msimu huu akiwa hajapata nafasi ya kuanza kwenye kikosi cha kwanza akiingia kama mchezaji wa akiba kwenye michezo miwiili pekee.

Ikiwa Pogba atabainika kuhusika na matumizi ya dawa hizo basi huenda akafungiwa kusakata soka kwa kipindi cha miaka miwili hadi Minne.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here