Home KITAIFA ROBERTINHO HANA WASI NA ZAMBIA, AWATUMIA WAMBA HAWA KUMALIZA KAZI

ROBERTINHO HANA WASI NA ZAMBIA, AWATUMIA WAMBA HAWA KUMALIZA KAZI

0
Simba Robertinho

Licha ya kuwahi kucheza na Power Dynamos ya Zambia na kupata matokeo mazuri, lakini Kocha mkuu wa Simba, Roberto Oliviera ‘Robertinho’ anaendelea kuwafatilia kwa umakini wapinzani wao hao.

Simba SC inaendelea na maandalizi ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Power Dynamos, utakaopigwa Jumamosi (Septemba 16), katika uwanja wa Levy Mwanawasa, Zambia.

Kocha Robertinho amesema kuwa amewapa wachezaji wake kutoka Zambia mbinu za kuwa wanaijua vizuri timu hiyo na wanachopaswa kufanya kuelekea katika mchezo huo.

Amesema wamefanikiwa kucheza na timu hiyo kwa kushinda anaimani katika mechi ijayo watakuja kivingine na kuwatumia wachezaji hao kutoa siri za Power Dynarmos.

“Haitakuwa mechi rahisi, kama tuliwafunga katika tamasha letu haitaleta maana kuwa watakuwa wepesi, ninaimani watakuja tofauti na vile walivyocheza awali kwa sababu haya mashindano.

“Binafsi presha kwa sababu tunao wachezaji wengi ambao wanawajua wapinzani wetu ambao tumecheza nao kabla ya msimu kuanza, lakini tunaamini watakuwa wamebadilika hivyo hawa ambao tupo nao naamini watatusaida,” amesema Robertinho.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here