Home KITAIFA SIMBA HAWAPOI MAWINDO YANAENDELEA SASA WAHAMIA HUKU

SIMBA HAWAPOI MAWINDO YANAENDELEA SASA WAHAMIA HUKU

0
BALEKE SIMBA

Baada ya kupata ushindi mnono dhidi ya Coastal Union katika mechi ya Ligi Kuu ya NBC, Wekundu wa Msimbazi Simba SC akili yao wanaielekeza kwenye mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Barani Afrika dhidi ya Power Dynamos.

Kwenye mechi ya awali wakiwa ugenini, Simba walipata sare ya goli 2-2 hivyo wanahitaji ushindi wowote, sare ya bila kufungana au ya goli moja ili kuweza kufuzu hatua ya makundi.

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba SC, Ahmed Ally, amesema mara baada ya mechi yao dhidi ya Coastal, wachezaji wamepewa mapumziko ya siku moja (leo Septemba 22) na kuanzia kesho ratiba rasmi ya mpango wao wa kuelekea mechi dhidi ya Power Dynamos ya Zambia itaanza.

“Tunapumzika leo na kusherehekea ushindi wetu wa Coastal Union, kesho tutatangaza ratiba rasmi ya kuelekea mchezo wetu wa marudiano dhidi ya Power Dynamos. Kikubwa sasa hivi akili yetu inahamia huko,” alisema Ahmed.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here