Kuelekea mchezo wa kimataifa Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Power dynamos FC dhidi ya Simba SC utakaochezwa Septemba 15 katika uwanja wa Levy Mwanawasa tayari timu mwenyeji ametangaza bei za tiketi kuelekea mchezo huo.
Bei ni kama ifuatavyo
jukwaa la Kaskazini, Kusini na Mashariki tiketi ni Kwacha 10 sawa na Sh1,231
Jukwaa na upande wa Magharibi ni Kwacha 30 sawa na Sh3,693.
VIP ni Kwacha 150 sawa na Sh18,467.
Na jukwaa la VVIP ni kwaajili ya mwaliko maalumu.
Uwanja wa Levy Mwanawasa unauwezo wa kubeba mashabiki 49,800 pungufu ya mashabiki 10,200 katika uwanja wa Benjamin Mkapa Dar es Salaam.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE