Home KIMATAIFA UMESIKIA SHERIA MPYA ZA ARTETA

UMESIKIA SHERIA MPYA ZA ARTETA

0
Arteta

Beki wa Arsenal, William Saliba amesema sheria mpya za Mikel Arteta zimesababisha wachezaji wa timu hiyo kuwa uhusiano mzuri zaidi nje na ndani ya uwanja.

Beki huyo wa kimataifa wa Ufaransa anaamini kutokana na sheria hiyo, wachezaji wa Arsenal wamejenga mawasiliano mazuri yaliyojenga urafiki, kwenye kikosi kinachowani mbio za ubingwa msimu huu.

Arteta aliandaa mpango wa kuja na sheria mpya wakati wa ziara ya kujiandaa na msimu mpya walipokwenda Marekani na imezaa matunda kwa mujibu wa Saliba.

“Kocha mara nyingi anazungumza na sisi kuhusu umoja na kuwa pamoja, sio tu mashabiki hata kwenye timu, mfano tulipokuwa kwenye ziara Marekani. Wakati wa kula kocha anabadilisha meza. Hatuchagui mtu wa kukaa naye wakati wa kula chakuka cha mchana au usiku. Amefanya hivyo ili kuwa na uhuru wa kuzungumza na kila mtu na nimeipenda sana hii sheria. Hiyo inasaidia kuongea na mtu ambaye hazungumzi naye kila mara,” alisema Saliba.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here