Home KITAIFA VIGOGO YANGA WAMWAGA PESA KWA MASTAA WAO

VIGOGO YANGA WAMWAGA PESA KWA MASTAA WAO

0
yanga hersi

Uongozi wa Klabu ya Yanga umeweka wazi kuwa utaendelea kumwaga pesa za maana za bonus kwa wachezaji kwaajili ya kuhakikisha kuwa timu hiyo inafanya vyema katika michuano ya kimataifa ambapo timu hiyo inaendelea kushiriki.

Aidha uongozi wa Yanga umeweka wazi kuwa msimu uliopita katika michuano ya kimataifa walifanikiwa kutumia zaidi ya shilingi Bilioni 1.2 katika kumwaga posho kwaajili ya wachezaji katika ichuano ya kimataifa.

Msimu uliopita ikumbukwe Yanga waliweza kutinga fainali ya kombe la Shirikisho Afrika ambapo walipoteza dhidi ya USM Algers katika mchezo wa fainali lakini pia walianzia katika ligi ya mabingwa na kutolewa katika hatua ya pili dhidi ya Al Hilal.

Akizungumza Afisa Habari wa Yanga Ally Kamwe alisema kuwa “Msimu uliopita Yanga ilitumia zaidi ya shilingi Bilioni 1.2 kwaajlili ya posho za wachezaji katika michuano ya kimataifa na msimu huu pia zitatumika pesa nyingi.

“Kama Yanga tulikusanya BILIONI 1.5 kutoka kwa wanachama, hivyo utaona pesa za wanachama zilitusaidia,hivyo niwaombe wanachama waendelee kuichangia timu yao ili tuwe na msuli wa pesa na tushindane na timu kubwa Afrika,” alisema Kamwe.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here