Home KITAIFA YACOUBA: HUYU AZIZ KI ATAWAUMIZA SANA

YACOUBA: HUYU AZIZ KI ATAWAUMIZA SANA

0
yacouba na aziz ki

Kiungo mshambuliaji wa Yanga, Stephanie Aziz KI yuko kwenye moto mkali kuliko msimu wa kwanza alipojiunga na timu hiyo kutoka Asec Mimosas, kiasi cha kumuibua nyota wa zamani wa timu hiyo, Yacouba Songne aliyefichua kuwa jamaa huyo amepania makubwa na ndio kwanza kazi imeanza.

“Nilipokuwa naondoka hapa niliongea naye nikamwambia mwaka wake wa kwanza hajafanya kitu kile ambacho watu walikuwa wanatarajia alitakiwa msimu huu afanye kweli, mimi namjua Aziz tangu nyumbani ni mchezaji wa kiwango kikubwa sana,”

“Alihitaji muda kuzoea ligi ya hapa unajua Aziz ni mchezaji mwenye ubora mkubwa wa ufundi na hapa ni tofauti soka la Ivory Coast unatakiwa kutumia sana nguvu, alikuwa anapata wakati mgumu kufanya vizuri walikuwa wanamkamia sana.”

“Aliniambia msimu huu atawasha moto na kwenye nguvu atahakikisha naye anatumia nguvu, nadhani mnaona sio rahisi kuchukua mpira kwake akiwa ameumiliki,”

“Bado hajafika mwisho, namfahamu vyema, msimu huu akiendelea kupandisha kiwango chake kama hivi atafanya makubwa sana, kitu kizuri naona makocha wake nao wanampa majukumu ambayo anayataka kucheza huru, hili litawasumbua sana wapinzani.”

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here