Home KITAIFA ALLY KAMWE ATOA KAULI HII BAADA YA YANGA KUPANGWA KUNDI D

ALLY KAMWE ATOA KAULI HII BAADA YA YANGA KUPANGWA KUNDI D

0
ally kamwe

Baada ya Yanga kupangwa kundi “D” ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL) ikiwa na Al Ahly, Belouizdad na Medeama Afisa Habari Yanga, Ally Kamwe ameandika kwenye ukurasa wake wa Instagram ya kwamba.

“Kundi D hakuna ubishi, hili ni Kundi Dume kweli, yupo Bingwa mtetezi, Al Ahly, yuko Belouizdad kutoka Algeria, yuko pia Medeama kutoka Ghana.

“Nini msimamo wetu kama Yanga sc? Hii ni nafasi nzuri kwetu kwenda kuipima project yetu ya michuano ya Kimataifa.

“Ni nafasi nzuri kwetu kuipima quality ya kikosi chetu dhidi ya Timu zenye Quality kubwa. Ni nafasi nzuri sana kwetu Yanga kwenda kuitangaza vyema Klabu yetu kwenye michuano ya Kimataifa.

“Siri yetu ya mafanikio ni ileile, kuungana na kushikamana kwa pamoja kama Taasisi. Kila mtu akicheza vyema kwenye Nafasi yake, INAWEZEKANA Daima Mbele Nyuma Mwiko,” ameandika Ally Kamwe.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here