Home KITAIFA AZIZI KI ATOA AHADI YA KIBABE YANGA

AZIZI KI ATOA AHADI YA KIBABE YANGA

0
Aziz Ki

Kiungo mshambuliaji wa Klabu ya Yanga, Stephane Aziz Ki, amesema licha ya kuwa kinara wa magoli katika Ligi Kuu ya NBC msimu huu, lakini hafikirii moja kwa moja kuwania Tuzo ya Ufungaji Bora, badala yake anataka kuona Yanga inatetea ubingwa wake.

Aziz Ki mwenye magoli sita, ndiye kinara wa ufungaji katika Ligi Kuu ya NBC msimu huu.

Katika mchezo uliopita ambao tulishinda magoli 3-2 dhidi ya Azam, Aziz Ki alifunga yote matatu ‘hat trick’.

Akizungumzia ishu ya kuwania ufungaji bora, Aziz Ki alisema: “Malengo yangu ni kuisaidia timu, sio kuwaza kiatu cha ufungaji bora.

“Mafanikio makubwa tunayoyatafuta hapa ni kubeba ubingwa, tukishalikamilisha hilo ndio tutaangalia kila mmoja nini amekipata kwenye mchango huo.”

Yanga kwa sasa inaongoza katika msimamo wa Ligi Kuu ya NBC baada ya kufikisha pointi 15, huku mapambano ya kutetea taji letu yakiendelea baada ya kulibebea kombe hilo mara mbili mfululizo msimu wa 2021-2022 na 2022-2023.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here