Home KIMATAIFA BUKAYO SAKA AONDOLEWA ENGLAND

BUKAYO SAKA AONDOLEWA ENGLAND

0
Saka

MSHAMBULIAJI wa Arsenal na timu ya Taifa ya Engalnd Bukayo Saka ameondolewa kwenye kikosi cha England kinachojiandaa na michezo ya kufuzu mashindano ya Euro dhidi ya Australia na Italia kutokana na majeraha.

Saka alikosekana kwenye ushindi wa 1-0 wa timu yake dhidi ya Manchester City Jumapili kutokana na jeraha la misuli ya paja.

Shirikisho la soka England ‘FA’ limethibitisha nyota huyo kuondolewa baada ya kufanyiwa uchunguzi na timu ya madaktari ya Uingereza.

England itamenyana na Australia tarehe 13 Oktoba, kabla ya kukutana na Italia katika mechi ya kufuzu kwa Euro siku nne baadaye.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here