Inaripotiwa kuwa klabu ya Chelsea ya England imefikia makubaliano ya kumuuza mshambuliaji wake Romelu Lukaku kujiunga na AS Roma ya Italia kwa mkataba wa kudumu mwishoni mwa msimu huu 2023-24.
Kwa sasa Lukaku anacheza Roma kwa mkopo akitoka Chelsea, yupo kwa mkopo mpaka mweishoni mwa msimu huu. Lukaku raia wa Ubeligiji amekuwa na mwanzo mzuri ndani ya klabu hiyo chini ya kocha Jose Mourinho, Lukaku amefunga mabao 7 kwenye michezo 8 aliyocheza msimu huu 2023-24.
Mkataba wa Chelsea na Lukaku unamalizika Juni 30, 2026. Lakini Lukaku hayupo tayari kuendelea kuichezea Chelsea na anataka kuondoka klabu hapo. Kwa mujibu wa ripoti the Blues wapo tayari kumuuza Lukaku kwa ada ya pauni milioni 37 zaidi ya Bilioni 113 kwa pesa ya Tanzania.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE