Home HABARI ZA AZAM FC LEO GAMONDI AITA MASHABIKI KUIMALIZA AZAM

GAMONDI AITA MASHABIKI KUIMALIZA AZAM

0

Kocha Mkuu wa YANGA SC, Miguel Gamondi amesema kikosi chake kipo imara kuvaana na matajiri wa Chamazi, Azam FC hapo kesho katika dimba la Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Gamondi amesema hayo leo Oktoba 22, 2023 jijini Dar es Salaam, katika mkutano na waandishi wa habari kuelekea mchezo huo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, ambapo amesema wamejipanga kuibuka na ushindi katika mchezo huo, huku akiomba mashabiki wa Yanga kuja kwa wingi uwanjani.

“Sisemi kuwa mashabiki wa Yanga watajaza uwanja ila nina uhakika watakuja kwa idadi kubwa kuipa nguvu klabu yao. Kwetu Amerika ya Kusini, mashabiki uwanjani ni mchezaji wa 12.” Ametamatisha hivyo Gamondi.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here