Home HABARI ZA YANGA LEO GAMONDI ATAJA KINACHOWAUMIZA YANGA

GAMONDI ATAJA KINACHOWAUMIZA YANGA

0
Gamondi aucho

MIGUEL Gamondi, Kocha Mkuu wa Yanga amesema miongoni mwa sababu zikizowafanya wakapoteza dhidi ya Ihefu ni Uwanja wa Highland Estate ambao haukuwa katika viwango.

Mateso ya kupoteza pointi tatu walikumbana nayo wachezaji na benchi la ufundi ugenini mara ya Kwanza msimu wa 2023/24.

Kocha huyo ameweka wazi kuwa wachezaji walikwama kutulia uwanjani na kucheza mpira vizuri jambo lililosababisha wakapoteza dhidi ya Ihefu.

“Kwenye mchezo wetu ulopita wachezaji walipata shida kutokana na uwanja nina amini mchezo wetu ujao tutafanya vizuri. Na pia maamuzi yalikuwa ni tofauti hilo lilionekana.

“Tuna mchezo dhidi ya Geita Gold ninatambua utakuwa na ushindani mkubwa na ambacho tunahitaji ni matokeo mazuri,”.

Miongoni mwa wachezaji wa Yanga waliofanya mazoezi ya mwishi ni Khalid Aucho, Clement Mzize, Djigui Diarra.

Kuhusu Uwanja wa CCM Kirumba ambao watautumia Leo dhidi ya Geita amesema bado hajaujua.

Kituo kinachofuata kwa Yanga ni Oktoba 7, Geita Gold v Yanga

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here