Home KIMATAIFA HAZARD ATANGAZA RASMI KUSTAAFU SOKA

HAZARD ATANGAZA RASMI KUSTAAFU SOKA

0
Edern Hazard

Mshambuliaji Eden Hazard ametangaza kustaafu soka la kulipwa.

Taarifa ya Hazard imeeleza “baada ya miaka 16 na zaidi ya mechi 700 kucheza, nimeamua kusitisha maisha yangu kama mchezaji wa kulipwa,”

“Wakati wa kazi yangu nilibahatika kukutana na wasimamizi wakuu, makocha na wachezaji wenzangu – asante kwa kila mtu kwa nyakati hizi nzuri.”

“Pia nataka kushukuru vilabu ambavyo nimechezea: LOSC, Chelsea na Real Madrid na shukrani kwa RBFA kwa uteuzi wangu wa Ubelgiji.”

“Shukrani za pekee kwa familia yangu, marafiki zangu, washauri wangu na watu ambao wamekuwa karibu nami katika nyakati nzuri na mbaya.”

“Mwisho, asante kubwa kwako, mashabiki wangu, ambao mmenifuata kwa miaka hii yote na kwa kunitia moyo kila mahali nilipocheza.”

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here