Home HABARI ZA AZAM FC LEO HUU HAPA MTAMBO WA MABAO NDAI YA AZAM FC

HUU HAPA MTAMBO WA MABAO NDAI YA AZAM FC

0
azam fc

KIUNGO mwenye kazi kubwa ndani ya Azam C kutengeneza mipango ya kusaka pointi tatu anaitwa Feisal Salum, Fei Toto.

Ni mtambo wa mabao ndani ya kikosi hicho tupo naye kwenye mwendo wa data namna hii:-

Mabao yake

Mabao matatu dhidi ya Tabora United mchezo uliochezwa Uwanja wa Azam Complex

Katika mchezo huo Fei Toto alipachika bao la kwanza dakika 3, 9 na ile kete ya tatu aliikamilisha dakika 13.

Katika mchezo huo ni mabao mawili alifunga kwa mguu wa kulia na bao moja alifunga kwa pigo la kichwa na yote alikuwa ndani ya 18.

Hat trick ya haraka

Nyota Fei Toto anashikilia rekodi ya kuwa nyota aliyefunga hat trick ya haraka zaidi ndani ya ligi kwa msimu wa 2023/24. Alifunga ndani ya dakika 12 kwenye mchezo huo ambao ulimalizika kwa kanuni.

Ikumbukwe kuwa kwenye mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Azam Complex Agosti 16 2023 kwa mujibu wa kanuni timu ikiwa na wachezaji (7) inaruhusiwa kucheza mchezo ndio maana waliruhusu mchezo uendelee licha ya kuwa Kitayosce walikuwa na wachezaji (8).Ambayo kwa sasa ni Tabora United hiyo ni kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Bodi ya Ligi Tanzania, Karim Boimanda.

Tabora United kwenye mchezo huo walikuwa hawajawa kamili kwa kuwa kuna wachezaji wao wengine walikuwa bado hawajakamilisha utaratibu wa usajili. Kwa sasa timu ipo kamili kuendelea na ushindani kwenye mechi za ligi.

Mkwakwani aliwaka

Nyota huyo katupia bao moja dhidi ya Coastal Union dakika ya 45 kwa mguu wa kulia ilikuwa ni Uwanja wa Mkwakwani.

Katika mchezo huo Coastal Union walikuwa wakisaka pointi mbele ya Azam FC mwisho waliyeyusha pointi tatu mazima.

Ni Fei alipachika bao la ushindi kwenye mchezo huo uliokuwa na ushindani akiwa ndani ya 18.

 

Mkali wa kulia

Ni mkali wa mguu wa kulia kwa kuwa kwenye mabao yake manne, ni mabao matatu kafunga kwa mabao matatu huku akifunga bao moja kwa pigo la kichwa.

Mabao yote kiungo huyo kafunga akiwa ndani ya 18. Uwanja wa Azam Complex kafunga mabao matatu na ugenini dhidi ya Coastal Union kafunga bao moja.

Mechi zake

Feisal kaanza kikosi cha kwanza kwenye mechi tano ndani ya kikosi hicho kinachonolewa na Kocha Mkuu, Yusuph Dabo.

Azam FC 4-0 Tabora United ngoma ilipigwa Agosti 16,2023,  Azam FC 3-1 Tanzania Prisons ilikuwa Uwanja wa Azam Complex, Azam FC 2-1 Singida Fountain Gate, Dodoma Jiji 0-0 Azam FC na Coastal Union 0-1 Azam FC.

Katika mechi hizo ilishinda mechi nne, sare moja na ukuta uliokota mabao mawili kibindoni walipokusanya jumla ya pointi 13.

Ni mabao 10 safu ya ushambuliaji ilifunga huku Fei akiwa namba mja kwa wenye mabao mengi ndani ya Azam FC.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here