Mshambuliaji wa zamani wa Simba na Taifa Stars, Emannuel Gabriel amesema:
“Kama Simba wanataka matokeo mazuri basi ni vyema kocha akawaanzisha Phiri na Baleke, ni wachezaji wanaompa matokeo mazuri na ukiangalia wamefanya vizuri kwenye mechi walizocheza.
“Kibu Denis anampa majukumu ambayo hayawezi kwa kumchezesha namba tisa, anamnyima uhuru wa kutembea, Bocco amwache kwanza benchi aingie timu ikipata matokeo mazuri na hawana cha kupoteza.
“Mechi mbili za mwisho za Simba zimeleta mwanga kuelekea dabi ingawa watani zao wapo vizuri, lakini kama kocha ataamua kutumia mshambuliajia mmoja basi tumwachie kazi yake na uamuzi wake huenda ukawa sahihi, ila kuimaliza Yanga ni kuwatumia Baleke na Phiri kwa pamoja.”
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE