Yanga wamepangwa kundi gumu CAFCL lakini wana nguvu ya kuvuka kwenda hatua ya robo fainali kwa sababu ya ile jeuri yao ya kushinda kwenye uwanja wowote iwe ugenini au nyumbani.
Faida nyingine kwa Yanga ni uthubutu hasa wanapokutana na timu za uarabuni, ni kama wanasema waarabu ni wababe lakini ngoja tuwaoneshe na hiyo imewasaidia kuwafunga USM Alger nyumbani kwao na wakaifunga Club Africain huko Tunisia.
Hizi rekodi zinaweza kuipa Yanga jeuri na nguvu kubwa kuelekea michuano ya CAFCL hatua ya makundi kwa sababu Kila mchezaji anajua kuwa timu yake haijawahi kumuogopa muarabu kwa Mkapa wala ugenini.
Jambo jingine zuri kwa Yanga ni kule kujua kuwa wanakutana na timu ngumu na hivyo kisaikolojia inawaingia kabisa kwamba wanahitaji maandalizi makubwa ya kutosha jambo ambalo ni zuri sana.