Home HABARI ZA SIMBA LEO JIONI KABISA MTU ALIPOTEZA AKIWA NYUMBANI

JIONI KABISA MTU ALIPOTEZA AKIWA NYUMBANI

0
Rekodi bora

REKODI iliyoandikwa zama zile ikiwa inaitwa Singida Big Stars kwa Simba kukwama kokomba pointi tatu ilivunjwa Oktoba 8 baada ya ubao kusoma Singida Fountain Gate 1-2 Simba.

Jioni kabisa mbabe alipatikana kutokana na bao lililofungwa ikiwa ni dakika 8 zilibaki kugota mwisho kwenye mchezo huo.

Ikumbukwe kwamba ilipokuwa ikiitwa Singida Big Stars ubao ulisoma Singida Big Stars 1-1 Simba,hapa tunakuletea baadhi ya kazi ilivyokuwa kwa mastaa hao:-

Beno Kakolanya

Okoa hatari dakika ya16, 17, 22, 23, 31, 72, alipiga pasi ndefu dakika ya 5, 7, 12, 18, 19, 28, 34, 41, 44, 68 alipiga pasi fupi dakika ya 15, 20, 21, 25, 38 alionyeshwa kadi ya njano dakika ya 21.

Aly Salim

Alitunguliwa bao moja dakika ya 52 aliokoa hatari dakika ya 20, 34, 53, 58. Alipiga pasi ndefu dakika ya 69 pasi fupi ilikuwa dakika ya 15, 32, 34, 38, 39.

Gadiel

Gadiel Michael alipewa jukumu la kurusha dakika ya 5, 14 aliokoa hatari dakika ya 6, 25, 28, 29, 59, alicheza faulo dakika ya 9 alipiga krosi dakika ya 24, 40.

Zimbwe Jr

Mohamed Hussen Zimbwe Jr aliokoa hatari dakika ya 33, 34, 41, 45 alipiga shuti ambalo halikuenga lango dakika ya 81.

Hamidu Wazir

Alipiga pasi fupi dakika ya 6, 7 alipiga pasi ndefu dakika ya 18, aliokoa dakika ya 5, 74, 78 alionyeshwa kadi ya njano dakika ya 78.

Kenedy Juma

Beki wa Simba aliokoa hatari dakika ya 8, 19, 31, 38, 67 alipiga pasi ndefu dakika ya 12 alikutwa kwenye mtego wa kuotea dakika ya 22.

Gyan

Nicolas Gyan alikomba dakika 64, alipiga faulo dakika ya 6 aliokoa hatari dakika ya 12 pasi ndefu alipiga dakika ya 28 nafasi yake ilichukuliwa na Nicolas Wadada.

Che Malone

Aliokoa hatari dakika ya 5, 13, 15, 24, 25, 28, 34 alipiga pasi ndefu dakika ya 6, alichezewa faulo dakika ya 31.

Andambwile

Aziz Andambwile alipiga faulo dakika ya 17, alipiga pasi ndefu dakika ya 18, 24, shuti ambalo lililenga lango alipiga dakika ya 33 alicheza faulo dakika ya 24, 54 alionyeshwa kadi ya njano dakika ya 54.

Ngoma

Fabrice Ngoma aliokoa hatari dakika ya 7, 15, 28, 29 alicheza faulo dakika ya 57.

Kagoma

Yusuph Kagoma alipiga pasi ndefu dakika ya 15, 24, alipiga shuti ambalo halikulenga lango dakika ya 31 aliokoa hatari dakika ya 44.

Kapombe

Shomari Kapombe aliokoa hatari dakika ya 41, alicheza faulo dakika ya 29 alipiga shuti ambalo lililenga lango dakika ya 21.

Bruno Gomes

Alipiga pasi fupi dakika ya 34 shuti ambalo lililenga lango alipiga dakika ya 20.

Kibu

Kibe Dennis alipiga shuti ambalo lililenga lango dakika ya 17, alikokota mpira dakika ya nne, alichezewa faulo dakika ya 3, 75, 78 alicheza faulo dakika ya 56 alitoa pasi ya bao kwa Saido Ntibanzokiza dakika ya 26.

Kaseke

Deus Kaseke alianzia benchi na alipoingia kipindi cha pili alipachika bao dakika ya 52 akiwa ndani ya 18 na alichezewa faulo dakika ya 68.

Bocco

Alikutwa kwenye mtego wa kuotea dakika ya 25 alipiga shuti lililolenga lango dakika ya 31 alikomba dakika 45 nafasi yake ilichukuliwa na Moses Phiri aliyepachika bao la pili kwa Simba dakika ya 82.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here