Kocha Mkuu wa timu ya Namungo ya mkoani Lindi, inayoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara, Cedric Kaze katangaza kuachia wadhifa huo.
Kaze ameandika kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Instagram kuwa: :Nimeamua kuanzia leo kujiuzulu kama Kocha Mkuu wa Namungo. Ningelipenda kuchukua fursa hii kuushukuru sana uongozi, wafanyakazi wenzangu wa benchi la ufundi na wachezaji kwa ushirikiano wao na kujitolea.
“ Nimalizie kwa kuwashukuru mashabiki ambao wamekuwa wakiniunga mkono kila wakati. Naitakia timu kila la heri kwa siku zijazo,” amesema Kaze.
Namungo imecheza michezo sita msimu wa Ligi Kuu Tanzania, ikiwa na pointi tatu tu na imefungwa michezo mitatu na sare michezo mitatu.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE