Home HABARI ZA SIMBA LEO KWA HALI HII YA SIMBA ROBERTINHO HANA MUDA MREFU

KWA HALI HII YA SIMBA ROBERTINHO HANA MUDA MREFU

0
Robertinho

Wakati Mashabiki wa Simba wakilalamika kiwango kibovu cha Simba katika michezo miwili ya hatua ya mtoano dhidi ya Power Dynamos ya Zambia.

Kuna waliokwenda mbali na kutaka Kocha Mkuu wa timu hiyo, Mbrazil Robertinho aoneshwe mlango wa kutokea.

Sasa mchambuzi wa michezo kutoka Clouds FM, Edo Kumwembe ametoa maoni yake kuhusiana na kiwango cha timu hiyo pamoja na hatma ya Kocha huyo,

“Nilichokiona katika mechi ya juzi ni kwamba Simba haiko fiti sana. Haipigi pasi kwa haraka. Haifungui nafasi kwa haraka zaidi. haikabi kwa haraka zaidi. Inaitwa pressing. Haifanyi mambo mengi kwa haraka. Mpira wa kisasa unataka wachezaji wafanye mambo mengi kwa haraka zaidi. Baada ya hapo ukiunganisha na vipaji vya wachezaji waliopo ni wazi kwamba utatawala mechi ya soka.

Inawezekana Robertinho kuna kitu anakitengeneza lakini kinaathiriwa na kocha wake wa viungo. Inawezekana kocha wa viungo kuna kitu anakifanya lakini mbinu za Robertinho hazifanyi kazi kwa wachezaji wake. Mwisho wa siku atakayeondoka ni Robertinho. Kwa namna ninavyoona mashabiki wameanza kupoteza imani naye

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here