Home HABARI ZA SIMBA LEO MAKUBWA! ROBERTINHO APANGUA KIKOSI, NIDHAMU YATAJWA

MAKUBWA! ROBERTINHO APANGUA KIKOSI, NIDHAMU YATAJWA

0
simba

Kocha wa Simba, Roberto Oliveira ‘Robertinho’ wala hana presha na mchezo wa marudiano akiwatumia salamu Al Ahly kuwa wanakwenda kupambana, huku akipangua kikosi.

Akizungumza amesema “Mimi siyo kocha wa kujilinda sijawahi kuwaza kucheza hivyo. Simba itacheza kwa nidhamu kubwa tukitambua ubora wa wapinzani wetu lakini tutawashambulia kwa akili,”

“Tunaweza kuwa na mabadiliko machache ya jinsi ya upangaji wa timu lakini kitu muhimu tutaingia na akili kubwa kupigania heshima ya Simba” amesema na kuongeza,

“Kila mtu ameona mchezo wa juzi. Kama tukiuanza kama tulivyoanza kipindi cha pili kuna kitu tutakitengeneza. Hakuna timu isiyofungika.”

“Kuna makosa tulifanya kipindi cha kwanza. Kuna wakati tulitengeneza urahisi wa Ahly kutushambulia bila sababu za msingi. Nafahamu tulipambana na timu kubwa yenye wachezaji bora lakini tutabadilika.”

Robertinho alikiri kwamba anaweza kuwa na mabadiliko ya kikosi katika mchezo huo utakaopigwa Oktoba 24, jijini Cairo nchini. Simba inatakiwa kushinda mchezo huo ili iweze kutinga hatua ya nusu fainali.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here